1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Mapambano ya kimadhehebu nchini Pakistan

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBX

Maafisa wa serikali nchini Pakistan wamesema,si chini ya watu 40 wameuawa na zaidi ya 70 wamejeruhiwa katika mapigano ya kimadhehebu yaliyozuka kati ya Waislamu wa Kisunni na Kishia kaskazini mwa nchi hiyo.Mapigano ya siku mbili yalizuka katika mji wa Parachinar kwenye wilaya ya North West Frontier iliyo karibu na mpaka wa Afghanistan.Mji huo unajulikana kwa mapambano ya kimadhehebu kati ya jamii za Wasunni na Washia. Amri ya kutotoka nje ilitangazwa siku ya Ijumaa katika eneo hilo,baada ya mapambano kuzuka kati ya makundi hayo mawili na vikosi vimetawanywa kurejesha hali ya utulivu.