1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad: Mripuko wa bomu la kujitolea mhanga lauwa si chini ya watu 15 nchini Pakistan

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCR3

Polisi nchini Pakistan wanasema mripuko wa bomu uliotekelezwa na mtu aliyejitolea mhanga umewauwa si chini ya watu 15 katika chumba cha mahakama. Polisi wanaamini hakimu na idadi kadhaa ya mawakili walikuwa miongoni mwa watu walouwawa pale bomu hilo liliporipuka pale mahakama hiyo ilioko katika mji wa kusini magharibi wa Quetta ilipokuwa ikisikiliza kesi. Kiasi ya watu 36, wengi wao wakiwa ni wakimbizi wa Ki-Afghanistan, wamekamatwa ili wahojiwe. Kumekuweko mlolongo wa mashambulio ya mabomu hivi karibuni huko Pakistan ambayo maafisa wa usalama wameyaunganisha na makundi yanayoendesha harakati katika maeneo ya kikabila na ambako wanamgambo wa Kitaliban wanaungwa mkono sana. Si wazi bado kama chama cha Taliban chenye siasa za Kiislamu kimehusika na shambulio hilo la Quetta.