1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Musharraf agoma kuondowa hali ya hatari

17 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImC

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan amegoma kuondowa utawala wa hali ya hatari nchini humo wakati akikutana na Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Negraponte.

Afisa wa rais wa Pakistan aliyekataa kutajwa jina lake amesema wanadiplomasia wa Marekani wameelezea wasi wasi wao juu ya kutokuwepo kwa hali ya utulivu wa kisiasa nchini Pakistan na wamemtaka Rais Musharraf achukuwe hatua kadhaa za kutuliza upinzani.

Miongoni mwa hatua hizo ni kumtaka Musharraf kuondowa utawala wa hali ya hatari mara moja,kujiuzulu wadhifa wa ukuu wa majeshi, kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa ratiba yake,kuondowa vikwazo dhidi ya vyombo vya habari na kuwaachilia wafungwa wa kisiasa.

Afisa huyo amesema Musharaf amesema anajaribu kwa kadri ya uwezo wake kufikiria kuondoa utawala wa hali ya hatari haraka iwezekanavyo lakini hakutaja tarehe yoyote ile.