1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Musharraf amuapisha waziri mkuu wa muda.

17 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImI

Rais wa Pakistan Pervez Musharaf amemuapisha waziri mkuu wa muda kuongoza nchi hiyo hadi katika uchaguzi wa mwezi Januari. Mwenyekiti wa baraza la seneti Mohammadmian Soomro aliapishwa katika Ikulu ya rais mjini Islamabad. Musharraf amesema kuwa ameiweka nchi hiyo katika njia kuelekea demokrasia. Katibu mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu Irene Khan amekanusha madai hayo ya Musharraf.

Chini ya sheria ya hali ya hatari itakuwa vigumu hivi sasa kwa vyombo vya habari kufanyakazi yao ya uhuru wa kujieleza. Ni vigumu kwa majaji na wanasheria kufanyakazi zao. Vipi unaweza kuwa na uchaguzi huru na wa haki chini ya hali hiyo.

Kuapishwa kwa Soomro kumekuja saa chache baada ya maafisa kumuacha huru kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto kutoka kizuizi cha nyumbani . Mwanadiplomasia wa Marekani John Negroponte amezungumza kwa simu na kiongozi wa upinzani nchini Pakistan Benazir Bhutto , muda mfupi baada ya kuwasili nchini humo, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni amesema. Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Negroponte amemtaka rais jenerali Musharraf kuondoa amri ya hali ya hatari aliyoiweka Novemba 3.