1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Pakistan yaonyesha ishara ya kuiachilia Kashmir.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmD

Pakistan imeonyesha ishara ya kuwa tayari kuacha madai yake katika eneo linalogombaniwa la Kashmir, iwapo India itakubali suluhisho la amani.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni ya India cha NDTV, rais Pervez Musharaff amesema kuwa hii itajumuisha pendekezo la utawala wa ndani chini ya uangalizi wa mataifa yote hayo mawili na kuyaondoa majeshi ya India kutoka katika eneo ambalo linatawaliwa na India katika Kashmir.

Lakini ameondoa uwezekano wa jimbo hilo kuwa huru.

India na Pakistan zimepigana vita mara mbili kuhusu jimbo la Kashmir tangu mwaka 1948.

Majadiliano juu ya suluhisho katika mzozo wa Kashmir yamekuwa yakiendelea tangu mwaka 2004.

Hakujakuwa na jibu kuhusiana na mpango wa utawala wa ndani uliotolewa na Musharaf kutoka India.