1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Serikali ya mpito imeapishwa Pakistan

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImN

Rais wa Pakistan,Jemadari Pervez Musharraf ameiapisha serikali ya mpito.Waziri Mkuu mpya Mohammadmian Soomro,ambae hapo zamani alikuwa mwenyekiti wa Bunge la Pakistan,ataiongoza serikali hiyo ya mpito hadi utakapofanywa uchaguzi mkuu mwanzoni mwa mwezi Januari.Rais Musharraf ameisifu hatua aliyochukua akisema hiyo ni njia inayoelekea kwenye udemokrasia.

Kwa upande mwingine,kiongozi wa upinzani,Benazir Bhutto ameipinga serikali hiyo mpya akisema kuwa imesaliti kwani imekula kiapo wakati wa hali ya hatari.Muda mfupi kabla ya hapo,Bhutto aliachiliwa huru kutoka kizuizi cha nyumbani.