1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Shambulizi limeua wanajeshi 4 Pakistan

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTo

Wanajeshi 4 wa Pakistan wameuawa katika shambulizi la bomu lililoripuliwa na mwanamgambo aliejitolea maisha muhanga.Wanajeshi 3 na raia 2 walijeruhiwa pia.Shambulizi hilo lilitokea karibu na mpaka wa Afghanistan,wakati wazee wa makundi ya kikabila walikuwa wakikutana na wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu katika eneo la machafuko la Kaskazini-Magharibi ya Pakistan. Wazee hao wanajaribu kupata maafikiano ya kuachiliwa huru kiasi ya wanajeshi 150 wa Pakistan.