1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Sheria ya kiislamu kuhusu ubakaji kubadilishwa

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsM

Bunge la Pakistan limeidhinisha mswada wa serikali,kubadilisha sheria kali za kiislamu za nchi hiyo kuhusu ubakaji na uzinifu.Kwa mujibu wa msemaji wa bunge,mswada huo wa sheria unawapa majaji busara ya kuamua ikiwa kesi ya ubakaji isikilizwe chini ya sheria ya uhalifu au ya kiislamu.Wabunge wa kiislamu wenye itikadi kali wamesusia kupiga kura wakisema,mabadiliko hayo ya sheria,yataifanya Pakistan kuwa kile waliochokiita „jumuiya ya ngono huru“.