1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Uchunguzi waendelea kuhusu mripua bomu nchini Pakistan.

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCX7

Maafisa wa Pakistan wanaendelea na uchunguzi kuhusu mripua bomu wa kujitoa mhanga aliyewaua watu kumi na watano na kuwajeruhi wengine zaidi ya thelathini.

Shambulio hilo la bomu ni la pili kutokea nchini humo tangu siku mbili zilizopita.

Mripuko huo uliotokea jana katika mji wa Peshawar, kaskazini mashariki mwa Pakistan, uliwalenga polisi waliokuwa wakilinda msikiti wa kishia.

Shambulio hilo lilitekelezwa wakati wafuasi wa madhehebu ya Shia walipoanza maadhimisho ya siku ya Ashura.

Siku ya Ijumaa, mtu mmoja alijiripua katika mkahawa mjini Islamabad na kusababisha kifo cha mlinzi aliyekuwa akimzuia kuingia kwenye mkahawa huo.