1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Upinzani wadai kuondolewa hali ya hatari

12 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJb

Upinzani nchini Pakistan leo hii umemtaka Rais Generali Pervez Musharraf kuondowa utawala wa hali ya hatari kwa kusema kwamba huenda wakaususia uchaguzi wa bunge unaokuja venginevyo haki za raia zinarudishwa kikamilifu na anajiuzulu ukuu wa majeshi.

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto amefuta uwezekano wa kuwa na mazungumzo zaidi na Rais Musharraf juu ya kushirikiana madaraka. Amewaambia waandishi wa habari katika mji wa Lahore kwamba chama chake cha PPP hakiwezi kushirikiana na mtu aliesistisha utawala wa katiba,alietangaza utawala wa hali ya hatari na kukandamiza vyombo vya mahkama.

Kauli hiyo ya Bhutto inakuja wakati chama chake kikijianda kufanya maandamano makubwa ya kupinga utawala wa hali ya hatari utakaoanzia mjini Lahore hadi Islamabad hapo kesho.

Musharraf hapo jana ametangaza uchaguzi utafanyika nchini humo mwezi wa Januari lakini amekataa kutangaza siku ya kuondolewa kwa utawala wa hali ya hatari.

Chini ya utawala huo wa hali ya hatari maelfu ya wapinzani wametiwa mbaroni, maandamano yamepigwa marufuku pamoja na kurushwa kwa matangazo ya vituo vya televisheni vya kibinafsi.