1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Wabunge wachagua rais mpya Pakistan

6 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7I8

Mahakama Kuu ya Pakistan imesema,uchaguzi wa rais unaruhusiwa kufanywa hii leo,lakini mshindi hatotangazwa mpaka itakapoamuliwa ikiwa Jemadari Pervez Musharraf anaweza kuchaguliwa tena wakati akibakia mkuu wa majeshi.

Musharraf ameahidi kujiuzulu jeshini ikiwa atachaguliwa tena kushika wadhifa wa urais.Jemadari Musharraf alinyakua madaraka takriban miaka minane iliyopita baada ya kumpindua Nawaz Sharif aliekuwa waziri mkuu.

Wachambuzi wa kisiasa wanaamini,Musharraf atashinda kwa urahisi,kufuatia kujiuzulu kwa zaidi ya wabunge 160 wa muungano wa upinzani unaoongozwa na mpinduliwa Sharif.

Kwa upande mwingine chama cha Pakistan People´s Party kimesema,hakitosusia uchaguzi huo,baada ya kiongozi wao Benazir Bhutto kusamehewa na Musharraf mashtaka ya rushwa.Musharraf na waziri mkuu wa zamani Bhutto,wanajadiliana njia ya kugawana madaraka.