1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Wafuasi wa Taliban wauawa Pakistan

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQR

Maafisa wa kijeshi nchini Pakistan wamesema, wamewaua wanamgambo 40 wanaowaunga mkono Wataliban,karibu na mpaka wa Afghanistan.Kwa mujibu wa msemaji wa kijeshi,helikopta zililenga vituo viwili vya wanamgambo katika eneo la Waziristan.Hapo awali,wanamgambo walikishambulia kituo cha ukaguzi na waliwatekanyara wanajeshi 12 katika Wilaya ya Kaskazini-Magharibi.Wakati huo huo waasi walionya kuwa wataanza kuwaua wanajeshi 200 waliozuiliwa mateka katika eneo hilo,tangu majuma mawili yaliyopita.