1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Wanamgambo 19 wameuawa Pakistan

22 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBg9

Vikosi vya usalama nchini Pakistan,vimewaua wanamgambo 6 wanaowaunga mkono Wataliban. Mapambano hayo yametokea kaskazini mwa jimbo la Waziristan,baada ya mapigano ya usiku kuuwa waasi 13.

Machafuko yameongezeka katika eneo hilo la hatari lenye makundi ya kikabila.Juma lililopita, wanamgambo katika eneo hilo karibu na mpaka wa Afghanistan,walitupilia mbali mkataba wa amani uliotiwa saini pamoja na serikali.

Siku ya Jumamosi,Rais George W.Bush wa Marekani alisema,inamsumbua kusikia kuwa kundi la al-Qaeda linaimarika katika eneo hilo la Pakistan ambako kuna makundi ya kikabila.