1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Wanasheria wapinga kurudishwa Sharif

11 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQn

Mawakili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif wamefunguwa kesi katika Mahkama Kuu leo hii wakipinga kurudishwa kwake nchini Saudi Arabia na hiyo kuanzisha malumbano mengine kati ya wanasheria na mtawala wa kijeshi wa Pakistan wakati akihaha kun’gan’gania madaraka.

Rais Generali Pervez Musharraf alimrudisha tena uhamishoni Sharif waziri mkuu aliempinduwa katika mapinduzi ya mwaka 1999 hapo jana masaa machache baada ya kutuwa Islambad akitokea London.

Wanasheria pia wanapanga kususia mahkama nchini kote Pakistan kupinga kurudishwa huko kwa Sharif kinyume na hukumu ya Mahkama Kuu kwamba kiongozi huyo wa zamani alikuwa na haki ya kurudi nchini Pakistan.