1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Watu 11 wauawa kwenye mapigano

4 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBm6

Watu takriban 11 wameuwawa na wengine 150 kujeruhiwa wakati wa mapambano baina ya maafisa wa usalama na wanafunzi kwenye msikiti mmoja mjini Islamabad Pakistan.

Machafuko hayo katika msikiti wa Lal Majid yalianza jana mwendo wa saa sita mchana wakati wanafunzi hao walipowakamata maafisa wanne wa polisi waliokuwa wakishika doria kwenye kituo cha upekuzi. Mapigano makali yalizuka na kuendelea hadi jana usiku.

Mzozo wa msikiti wa Lal Majid au msikiti mwekundu ulianza mnamo mwezi Februari mwaka huu wakati maelfu ya wanafunzi wenye siasa kali ya kiislamu wafuasi wa msikiti huo, walipojaribu kulazimisha utawala wa kiislamu wa kitaliban miongoni mwa wakaazi wa mjini Islamabad.