1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD. Waziri ajiuzulu kupinga njama ya rais Musharaf kutaka kubakia madarakani

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBV2

Waziri anayehusika na teknolojia ya habari nchini Pakistan, Ishaq Khan Khakwani, amejiuzulu kupinga mpango wa rais Pervez Musharaf kutaka kuendelea kubakia madarakani.

Waziri huyo amesema anajiuzulu wadhifa wake lakini ataendelea kuwa mtiifu kwa chama tawala cha Paksitan Muslim League Quaid, PML- Q.

Waziri Ishaq ametaka kufanyike mdahalo wa kitaifa utakaovijumulisha vyama vya kisiasa vya upinzani.

Wakati huo huo, mbunge Ali Hassan Gilani, ambaye ni katibu wa bunge anayehusika na maswala ya sayansi na teknolojia, amesema anakihama chama tawala na kujiunga na chama cha waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif.