1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Waziri wa kigeni wa Uingereza akutana na rais Musharaf

26 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBez

Waziri mpya wa mashauri ya kigeni wa Uingereza, David Miliband, amefanya mazungumzo na rais wa Pakistan, Pervez Musharaf, mjini Islamabad.

Baada ya mkutano huo, Miliband amesema Uingereza ina maslahi katika uthabiti wa Pakistan na juhudi za Musharaf kupambana na wanamgambo wa makundi ya Taliban na al Qaeda.

Waziri Miliband amesema vita dhidi ya ugaidi si mgongano baina ya ustaarabu wa nchi za magharibi na za kiarabu.

´Hizi ni juhudi kati ya watu wa nchi, kabila na dini mbalimbali wanaoamini kwamba ni sawa watu wa kabila na dini tofauti watafute njia za kuishi pamoja na kuwatenga wale wanaoonekana kutaka kuhatarisha njia zetu zote za kuishi.´

Waziri David Miliband aliwasili mjini Islamabad akitokea nchini Afghanistan ambako alifanya ziara ya siku mbili.

Habari zaidi zinasema Pakistan imefanya jaribio la kombora aina ya Babur linaloweza kwenda kwa umbali wa kilomita 700. Jeshi la Pakistan limesema jaribio hilo limefaulu lakini haikubainika wazi ikiwa Pakistan iliifahamisha India juu ya jaribio hilo.

India na Pakistan zina makubaliano ya kujulishana iwapo zinafanya majaribio ya makombora aina ya balistik lakini sio makombora ya masafa marefu.