1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Benazir Bhuto kurejea Pakistan mwezi ujao

14 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPn

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan bibi Benazi Bhuto ametangaza kwamba atarejea nchini humo mwezi ujao wa Oktoba.

Bibi Bhuto atarejea nchini Pakistan baada ya kuishi uhamishoni kwa zaidi ya miaka minane.

Kwa mujibu wa naibu mwenyekiti wa chama cha Pakistan People’s Party Makhdoom Amin Faheem, bibi Benazir Bhuto atawasili mjini Karachi tarehe 18 mwezi wa Oktoba.

Waziri huyo mkuu wa zamani inaripotiwa kwamba amekuwa akifanya mazungumzo na rais Pervez Musharraf wa Pakistan juu ya kugawana madaraka.

Jenerali Musharraf anatarajia kurejea tena madarakani baada ya kukamilisha awamu yake ya pili ya kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Pakistan.

Uchaguzi nchini humo umepangwa kufanyika katika muda wa wiki nne zijazo.