1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Bhutto afuta ziara yake ya Dubai kukiwa na tetesi Musharaf atatangaza hali ya hatari

1 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ar

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistana Benazir Bhutto amefuta ziara yake ya kwenda Dubai kufuatia ripoti kwamba kuna uwezekano war ais Pervez Musharraf akatangaza hali ya hatari ikiwa mahakama itatoa uamuzi dhidi ya uhalali wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Mahakama kuu nchini Pakistan inatarajiwa kutoa uamuzi baadae wiki hii juu ya ikiwa uchaguzi war ais uliopita ulifanyika kwa mujibu wa katiba.

Rais Musharraf aliahidi kujiuzulu kama mkuu wa jeshi kufikia katikati ya mwezi Novemba ikiwa angeshinda uchaguzi lakini hajasema atacchukua uamuzi gani endapo mahakama itabatilisha ushindi wake.Hali ya kisiasa katika taifa hilo imekuwa tete katika miezi ya hivi karibuni.Waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto alirejea Pakistan baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka minane na saa chache baada ya kuwasili mjini Karachi alikaribishwa na shambulio la bomu lililosababisha mauji ya watu 139 na wengine wengi wakajeruhiwa.