1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Bhutto atokea hadharani

22 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dj

Aliekuwa waziri mkuu wa Pakistan bibi Benazir Bhutto ametokea hadharani kwa mara ya kwanza tokea aponee chupu chupu shambulio la kutaka kumwuua.

Bibi Bhutto alirejea Pakistan wiki jana baada ya kuishi katika hifadhi , nje kwa muda wa miaka minane kwa hiari yake.

Mwanasiasa huyo amezitaka Marekani na Uingereza zisaidie katika uchunguzi wa jaribio la kutaka kumwuua . Watu wapatao 140 waliuawa katika jaribio hilo.