1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Jaji mkuu aendelea kupambana na rais Musharraf nchini Pakistan

5 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4d

Jaji mkuu aliefukuzwa kazi nchini Pakistan bwana Iftikhar Mohammed Choudry leo ameenda katika mji wa Lahore mashariki mwa nchi hiyo ili kuwahutubia watu wanaomwuunga mkono katika mapambano yake dhidi ya rais Pervez Musharraf aliemfukza kazi jaji mkuu huyo kwa madai kwamba alikuwa anatumia vibaya wadhifa wake.

Maandamano makubwa yamefanyika kumwuunga mkono jaji mkuu huyo tokea rais Musharraf alipochukua hatua ya kumkataza kufanya kazi kama jaji mkuu.

Bwana Choudry anatarajiwa kuwahutubia wanasheria na watu wengine wanaomwuunga mkono katika mji wa Lahore.