1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Jaji mkuu kujitenga na uamuzi wa kesi ya uhalali wa ushindi wa Rais Musharraf

17 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ew

Jaji mkuu nchini Pakistan anakataa kuhusika na shughuli ya kutoa uamuzi kufuatia madai ya uhalali wa ushindi wa Rais Pervez Musharraf yaliyowasilishwa kwenye mahaka kuu na vyama vya upinzani.Wanasiasa wa upinzani wanadai kuwa Jenerali Musharraf hakupaswa kugombea tena urais kisheria kwasababu bado hajajiuzulu kama mkuu wa majeshi.Uchaguzi wa rais ulifanyika tarehe sita mwezi huu.Serikali kwa upande wake inashikilia kuwa uchaguzi huo ulitimiza sheria ila mahakama kuu itamtangaza mshindi rasmi baada ya malalamiko hayo ya upinzani kuchunguzwa.

Wakati huohuo waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto anathibitisha kuwa anarejea nchini mwake hapo kesho ili kushiriki katika kampeni za uchaguzi unaopangwa kufanyika mwaka ujao.

''Kurejea kwangu kunaashiria mabadiliko ya mfumo wa kisiasa kwa wakazi wa nchi ya Pakistan kutoka udikteta hadi demokrasia…..kumalizika kwa kunyanyaswa na watu kujitegemea……kutoka ghasia hadi amani''

Mwanasiasa huyo wa chama kikubwa cha upinzani cha Pakistan Peoples Party ,PPP alienda uhamishoni zaidi ya miaka minane iliyopita alipokabiliwa na mashtaka ya rushwa.

Bi Bhutto atapewa ulinzi na polisi alfu 20 pamoja na kulakiwa na wafuasi takriban milioni moja.