1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Jaji mstaafu atangaza kugombea uchaguzi wa rais

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMx

Jaji mstaafu wa mahakama kuu ya Pakistan bwana Wajihuddin Ahmed na mpinzani mkubwa wa utawala wa kijeshi ametangaza nia yake ya kumpinga rais Pervez Musharraf katika uchaguzi wa tarehe 6 mwezi Oktoba.

Licha ya kutokea machafuko katika eneo la mahakama kuu mjini Islamabad na mapambano baina ya polisi wa kutuliza ghasia na wafuasi wa upinzani, Wajihuddin Ahmed amesema amelikubali ombi la wanasheria ambao wanaendeleza harakati za kumpinga jenerali Musharraf.

Hata hivyo bwana Ahmed ana nafasi ndogo ya kushinda kwani rais wa Pakistan anachaguliwa na wabunge ambao wako chini ya ushawishi mkubwa wa jenerali Musharraf.