1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Maandamano yafanyika kumpiga Rais Musharraf

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCk

Zaidi ya wapinzani elfu 4 wa rais Pervez Musharraf wa Pakistan wamefanya maandamano makubwa katika mitaa ya jijini la Islamabad kupinga uamuzi wa rais huyo kumsimamisha kazi jaji mkuu wa nchi hiyo.

Maandamano hayo ya wanaharakati wa kisiasa na wanasheria yalifanyika pia nje ya mahakama kuu ya nchi hiyo ambapo kesi ya jaji huyo mkuu inasikilizwa.

Rais Musharraf alimsimamisha kazi jaji mkuu huyo mwenye msimamo, Iftkhar Mohamed Chaudhry mwezi uliyopita kwa tuhuma kuwa alifanya upendeleo kwa mwanaye wa kiume.

Makamu wa Rais wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini humo cha PPP, Makhdoom Amin Fahim aliwaambia waandamanaji kuwa ni lazima wa shirikiane katika kumuondoa Rais Musharraf ambaye amemuita kuwa ndiye chanzo cha matatizo nchini Pakistan.