1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Makombora yaua watu saba Pakistan

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfd

Watu saba wamekufa na wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi ya makombora huko Kaskazini Magharibi mwa Pakistan.

Polisi wamesema kuwa nyumba, maduka na msikiti vilishambuliwa na makombora manne ambayo inahisiwa yalifyatuliwa na wanamgambo wa kiislam.

Hali ya usalama nchini Pakistan imezidi kuwa mbaya, toka majeshi ya serikali yalipovamia na kuwafurusha wanamgambo wa kiislam kwenye msikiti mwekundu mjini Islamabad mapema mwezi huu.

Wakati huo huo, Pakistan kwa mara nyingine tena imepinga shambulizi lolote litakalofanywa na Marekani dhidi ya Osama Bin Laden iwapo itathibitika kuwa yuko nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Khurshid Kasuri amesema kuwa nchi hiyo inahofu kuwa harakati zozote zitakazofanywa na Marekani zitasababisha maafa makubwa kwa raia.

Hata hivyo Marekani imesema kuwa hakuna kitakachoizua katika kumsaka Osama Bin Laden.