1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Mazungumzo ya Bi Bhutto kufutiwa mashtaka yakwama

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKP

Mazungumzo ya kugawana madaraka kati ya Rais Pervez Musharraf wa Pakistan na Waziri Mkuu wa zamani Benazir Bhutto yamekwama huku wandani wake wakipinga hatua ya kufutwa kwa mashtaka ya rushwa yanayomkabili.

Serikali ya Pakistan ilitangaza hapo jana kuwa itafuta mashtaka ya rushwa yanayomkabili Bi Bhutto jambo litakalomwezesha kushiriki katika uchaguzi wa Jumamosi.

Kulingana na Bi Benazir Bhutto kauli hiyo si sahihi. Kiongozi huyo anaonya kuwa mkwamo wa kisiasa unaoendelea kabla uchaguzi wa mwishoni mwa juma huenda ukasababisha ghasia.

Kiongozi huyo wa zamani anapanga kurejea nchini mwake Otkoba 18 na kudai kufutiwa mashtaka yanayomkabili kabla hilo.Benazir Bhutto alikuwa Waziri mkuu wa Pakistan mwaka 88 hadi 90 na katika kipindi cha pili kuanzia mwaka 93 hadi 96.

Kulingana na naibu mwenyekiti wa chama cha Pakistan People PPP ambacho pia ni chama cha Bi Bhutto hatua ya kufutiwa mashtaka haitoshi.Duru za chama tawala zinaeleza kuwa huenda kikapinga hatua hiyo mahakamani endapo Rais Musharraf atatangaza uamuzi utakoaofanikisha hatua ya kufutwa kwa mashtaka yanayomkabili Bi Benazir Bhutto.