1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Musharaff atangaza rasmi kuwania urais

20 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOA

Rais Pervez Musharraf ametangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi ujayo pamoja na kukabiliwa na pingamizi lililoko katika mahakama kuu dhidi yake.

Tume ya uchaguzi nchini Pakistan imetangaza tarehe sita mwezi ujayo kuwa ni siku utakaofanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Kesi iliyofunguliwa katika mahakama hiyo inapinga uhalali wa Musharraf kuendelea kuwa mkuu wa majeshi huku akitaka kugombea urais.

Hata hivyo wafuasi wake wamesema kuwa kiongozi huyo atang´atuka katika cheo cha ukuu wa majeshi iwapo atashinda kipindi kingine cha pili cha uongozi.