1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Musharraf azidi kupata wapinzani kuwania urais

27 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBML

Chama cha Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto kimemteua makamu wake wa rais Makhdoom Amin Fahim kuwania urais wan chi hiyo katika uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.

Chama hicho kimesema kuwa kiongozi wa kijeshi wa Pakistan General Pervez Mushararf ameshindwa katika vita dhidi ya ugaidi.

Generali Musharraf ambaye ni mshirika mkubwa wa Marekani katika vita dhidi ya ugaidi, anakabiliwa na upinzani wa wagombea wawili katika uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 6 mwezi ujayo.

Bi Benazir Bhutto anatarajiwa kurejea nchini Pakistan mwezi ujayo kutoka uhamishoni.