1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Onyo la mwisho latolewa dhidi ya wenye itikadi kali

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkc

Maofisa nchini Pakistan wametoa kile walichokitaja kuwa onyo la mwisho kwa waislamu wenye itikadi kali waliojificha ndani ya msikiti mwekundu uliotekwa mjini Islamabad.

Hata hivyo kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali Adbul Rashid Ghazi na wafuasi wake hawajaridhia kusalimu amri kufuatia vitisho vilivyotolewa na rais Parvez Musharraf ambaye amewataka mamia ya watu walioko ndani ya msikiti huo kujisalimisha au kuuwawa.

Insert Otone

Hali ya wasiwasi ilianea zaidi hapo jana wakati vikosi vya serikali vilipozidisha mashambulio na kubomoa sehemu za msikiti huo ili kuwakomboa wanawake na watoto.

Watu 21 wameuwawa tangu kuanza kwa mvutano huu siku ya jumanne.Wanafunzi wa msikiti huo wanataka kuanzishwa kwa sharia za kiislamu katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad.