1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Rais wa Pakistan aondoa uwezekano wa kutangaza hali ya hatari

9 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBan

Rais wa Pakistan ameamua kutotangaza hali ya hatari nchini humo.Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP taarifa hiyo imetolewa na afisa mmoja wa ngazi ya juu serikali aliyekataa kutajwa jina.

Taarifa za awali zilieleza kwamba rais wa Pervez Musharaf huenda angetangaza hali ya hatari wakati wowote.ilidokezwa kwamba waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice amefanya majadiliano marefu kwa njia ya simu na rais Musharraf kuhusiana na hali hiyo.Hii ilitokea baada ya waziri wa habari wa Pakistan kutangaza kwamba Musharraf huenda akaweka hali ya hatari kufuatia kuzorota kwa usalama katika eneo tete la kaskazini magharibi karibu na mpaka na Afghanstan.

Wakati huohuo Mkutano juu ya kukabiliana na kundi la Taliban unaendelea huko Afghanstan bila ya rais Pervez Musharaf aliyefutilia mbali ziara yake ya kwenda Afghanstan kuhudhuria kikao hicho.

Kikao hicho kinachojulikana kama Jirga yaani kikao cha baraza la kijamii kinalengwa kutatua mizozo na kupambana na ongezeko la uasi wa kundi la Taliban waziri mkuu Shaukat Aziz amemuwakilisha rais Musharaf kwenye mkutano huo.Hakuna sababu zozote zilizotolewa juu ya kutofika kwa bwana Musharraf.