1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Serikali yakataa mazungumzo na viongozi wa Lal Masjid

6 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlK

Naibu Kiongozi wa Lal Masjid Abdul Rashid Ghazi anakataa kujisalimisha bila masharti na kwamba yeye na wafuasi wake wako tayari kupoteza maisha yao kwasababu ya dini.Msikiti huo umezingirwa na majeshi ya serikali ikiwa ni siku ya tatu.

Kauli hiyo ni kinyume na alivyotangaza awali kuwa yuko tayari kujisalimisha.Majehsi ya serikali yanaendelea kushambulia msikiti huo kwa risasi na vifaa vya milipuko japo kuzuia umwagikaji wa damu.Serikali kwa upande wake inajaribu kuzuia maafa makubwa kutokea kwani hilo litaaharibu sifa ya Rais Pervez Musharraf.Hata hiyo serikali inakataa kufanya mazungumzo zaidi.Tariq Azeem Khan ni naibu waziri wa habari na mawasiliano nchini Pakistan

''Serikali kamwe haitafanya mazungumzo mengine yoyote.Muda mwingi umeshapita sasa wakati tunajaribu kuwashawishi waliojificha msikitini kujisalimisha.Wakati wote tumesisitiza kupatikana suluhu kwa njia ya amani ya majadiliano.Kwahiyo sharti wajisalimishe bila masharti yoyote ''

Majeshi ya serikali yalizingira msikiti wa Lal siku ya jumatano ikiwa ni siku moja baada ya majeshi ya serikali na wafuasi wa msikiti kupambana.Wafuasi hao wanalazimisha kutumiwa kwa sheria ya Taleban jambo lililosababisha ghasia kutokea na kusababisha vifo vya watu 19.