1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:watu 15 wameuwawa katika shambulio la kujitoa muhanga

1 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBL6

Takriban watu 15 wameuwawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na kituo cha polisi nchini Pakistan.

Watu 19 wamejeruhiwa katika shambulio hilo ambapo mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliyevalia vazi la kike la Burka alipoulenga msafara wa kijeshi karibu na mji wa kasakzini magharibi wa Bannu ulio katika eneo la mpakani kati ya Pakistan na Afghanistan.

Shambulio hilo la leo ni miongoni mwa mfululizo wa mashambulio tangu vikosi vya serikali vilipouvamia msikiti mwekundu wa mjini Islamabad.

Shambulio hilo pia limetokea siku chache tu baada ya mahakama mjini Islamabad kutoa ruhusa kwa jenerali Pervez Musharraf kugombea tena wadhfa wake huku akiwa bado anashikilia madaraka ya kijeshi.