1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel itasitisha ujenzi wa makazi katika ardhi ya Wapalestina

19 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJL8

Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert amesema,Israel haitojenga makazi mapya ya Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina.Katika kikao cha baraza la mawaziri Olmert alisema,makazi yote yaliyojengwa bila ya vibali yatabomolewa.Israel kwa kuchukua hatua hiyo inataka kutekeleza sharti mojawapo muhimu la mchakato wa amani wa jumuiya ya kimataifa,ambao pia hujulikana kama „Roadmap“. Mpango huo wa amani wa Mashariki ya Kati,unatoa mwito wa kusitisha harakati za kujenga makazi ya Wayahudi.

Mkutano wa amani wa Mashariki ya Kati ulioitishwa na Rais wa Marekani George W.Bush umepangwa kufanywa juma lijalo mjini Annapolis,Maryland nchini Marekani.