1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kujenga nyumba mpya katika ardhi ya Wapalestina

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfdr

Jerusalem. .

Israel imefichua mipango ya kujenga zaidi ya nyumba 70 mpya katika ardhi wanayoikalia mashariki ya Jerusalem na ukingo wa magharibi mwaka ujao.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameushutumu mpango huo , akisema upanuzi wa makaazi ni kikwazo kikubwa katika majadiliano ya amani ambayo yanatarajiwa kuanza tena leo Jumatatu.

Naye msemaji wa serikali Abou Amri amesema kuwa mpango huo utaondoa maana katika mkutano wa Annapolis.

Israel imetangaza katika mkutano wa amani uliodhaminiwa na Marekani mjini Annapolis mwezi uliopita kuwa itaendelea kuwa mkweli katika mpango wa amani unaofahamika kama road map. Mpango huo ni pamoja na kusitishwa kwa upanuzi wa makaazi ya Wayahudi . Lakini serikali ya Israel imesema kuwa nyumba hizo mpya katika moja ya makaazi hayo zilikuwa ni sehemu za mpango uliotayarishwa miaka saba iliyopita na sio sehemu ya mpango huo wa amani wa roadmap.