1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kupunguza nafuu za wafungwa wa kipalastina

Oumilkher Hamidou29 Machi 2009

Wafungwa wa kipalastina hali zao jela zinabidi zilingane na zile za Gilad Shalit

https://p.dw.com/p/HMHP

Jerusalem:

Wakuu wa jela nchini Israel wameanza kuzidisha makali ya sheria za kushikiliwa wafungwa wa chama cha itikadi kali cha Hamas-hayo ni kwa mujibu wa duru za serikali mjini Jerusalem.Kiongozi wa shughuli za tawala katika jela Benny Kaniak ameiarifu serikali kwamba jela "zimeanza kutia njiani baadhi ya mapendekezo ya kamisheni iliyoundwa kufuatia juhudi za waziri wa sheria anaemaliza wadhifa wake Daniel Friedman.Kamisheni hiyo imeundwa kwa lengo la "kupunguza nafuu wanazopewa wafungwa wa kutoka makundi ya Hamas na Jihad.Wiki ijayo kamisheni hiyo inapanga kuikabidhi serikali mpya ya Israel orodha kamili ya mapendekezo yake.Wafungwa 11 elfu wa kipalastina wanashikiliwa katika jela za Israel,na maelfu kati yao ni wafuasi wa Hamas.Hatua hizo zimetangazwa katika wakati ambapo mazungumzo ya kubadilishana wafungwa wa kipalastina na  mwanajeshi wa Israel Gilad Shalit,aliyetekwa nyara mwaka 2006 na Hamas yamekwama mjini Cairo nchini Misri.