1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Hizbollah

15 Julai 2008

Israel na Hizbollah zabadilishana leo wafungwa.

https://p.dw.com/p/Ed3T

Baada ya Baraza la mawaziri la Israel kuidhinisha jana mpango wa kubadilishana wafungwa na chama cha Hizbollah cha Lebanon, wafungwa hao wanatazamiwa kubadilishwa hii jumatano hii.

Waziri mkuu Ehud Olmert wa Israel na mawaziri wengine 21 waliupigia kura mpango huo licha ya upinzani mkali kutoka kwa idarasa ya usalama wa ndani ya Israel "Shin Bet" na Idara ya ujasusi ya Israel Mosad.Pia mawaziri 3 waliupinga mpango huo.

Kubadilishana kwa maiti za wanajeshi wa Israel kwa wafungwa wa kipalestina kuna mila na desturi zake za muda mrefu.Na hii ni sawa na kutumika Ujerumani kama mpatanishi .Hali imekuwa hivyo hata mara hii.

Baadae rais Shimon Peres alitia saini yake hati ya msamaha kwa Samir Kuntar,mmoja kati ya wafungwa 5 wa Lebanon aliekua muda mrefu zaidi kizuizini.

Rais Perez alisema , msamaha wake ni kwa sharti kuwa Hizbollah, nchini Lebanon inawaacha huru wanajeshi 2 wa kiisraeli Eldad Regev na Ehud Goldwasser.

kuntar akitumikia kifungo cha vipindi mbali mbali kwa pamoja katika gereza la Israel kwa kufanya hujuma ya 1979 huko kaskazini mwa Israel.katika shambulio hilo yeye na wenzake waliwaua askari polisi 2 wa Israel pamoja na baba na msichana wake wa miaka 4 waliomchukua mateka.

Mahkama ya sheria ya Israel iliyakataa malalamiko ya dakika ya mwisho kutoka kwa ukoo mmoja wa askari hao kuzuwia mpango huu kusonga mbele.

Malori 9 ya chama cha Msalaba Mwekundu Ulimwenguni yamewasili Israel kutoka nchi jirani ya Jordan kuwasafirisha hadi Lebanon baadhi ya maiti 199 za wapiganaji wa Lebanon zilizokuwapo katika makaburi maalumu za maadui walifariki.

Wajumbe hao wa chama cha msalaba mwekundu walikutana jana asubuhi na wafungwa hao 5 wa Lebanon wanaoachwa huru hii leo katika gereza la Hadarim la Israel kabla mpango huo wa kubadilishana wafungwa leo kuanza.

Kwa muujibu wa mapatano Israel inapaswa kukabidhi maiti hizo 199 ili ikabidhiwe nayo wanajeshi wake 2 Regev na Goldwasser ambao wanafikiriwa wamefariki dunia.

Wanajeshi hao 2 walitekwa katika hujuma ya kuvuka mpaka iliofanywa na wapiganaji wa Hizbollah ambayo ilichochea vile vita vya mwezi mzima na Lebanon hapo 2006 bila kupelekea kuachwa kwao huru.

Idara za usalama za Israel Shin Bet na Mossad zinaupinga mpango wa kumuacha huru Kuntar kwa kuwa zinahofia itakua kupoteza nafasi ya mwisho ya kujipatia taarifa madhubuti juu ya mwanahewa anatafutwa wa kiisrael,Ron Arad.

Ndege ya Arad iliangushwa katika anga la Lebanon hapo 1986.Alizuwiliwa kwa miaka mingi na chama cha Amal cha Lebanon na halafu akatoweka bila kujilikana alipo.

Ingawa hakuna anaeamini kuwa Arad bado anaishi,Israel iliendelea na juhudi za kumrejesha nyumbani au kujua hatima yake.Mara hii yaonesha kufikiwa shabaha hiyo.

Hizbolla imetoa ripoti ambamo imearifu kuwa Arad kiasi cha miaka 2 iliopita tangu kukamatwa yamkini ameuliwa.

Ripoti hii ilikabidhiwa Israel na mjumbe wa kijerumani aliekua anatumika pande zote mbili.Mtumishi wa zam,ani wa Idara ya usalama ya Ujerumani BND Gerhard Konrad akipatanisha wakati ule baina ya Hizbollah na Israel na ndie alieandaa mpango wa hii leo wa kubadilishana wafungwa na maiti.

Ingawa ,fungwa wa muda mrefu Kuntar ni wa madhehebu ya Druz na sio Shiia, Hizbollah kilichopigana vita nchini Lebanon na Israel 2006, kilishikilia kuachwa kwake huru kuwa lazima kwa sababu hajakuwamo ndani ya ule mpango wa 2004 wa kubadilishana wafungwa.