1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na maskani

9 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CZLA

JERUSELEM:

Makamo-waziri mkuu wa Israel akijibu leo ila zilizotolewa na Marekani juu ya mipango ya Isarel ya kujenga maskani zaidi ya wayahudi katika eneo la mji wa Jeruselem lililokaliwa na Israel,alisema sehemu ya mji huo, lazima iachwe mikononi mwa wapalestina ili kukwepa kutoungwamkono na Marekani.

Hatahivyo, Haim Ramon aliambia Radio Israel kuwa Israel, haitaachana na maskani za wayahudi kule ambako mpango wa majenzi uliotangazwa wiki iliopita ulizusha hasira za wapalestina na onyo kutoka kwa waziri wa nje wa Marekani Dr.Condoleeza Rice.dr.Rice alisema mpango huo unahatarisha kuchafua utaratibu wa amani aliosaidia kuufufua huko Annapolis,mwezi uliopita.