1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Palestina hatari ya machafuko kwa mara ya tatu

13 Novemba 2014

Kwa mara ya pili sasa Wapalestina tayari wameshazua vuguvugu za upinzani dhidi ya Israel zinazojulikana kama 'Intifada'. Na kwa sasa vurugu mpya baina yao huenda zikazua vuguvugu la upinzani kwa mara nyengine ya tatu.

https://p.dw.com/p/1DmK8
Israel - Sperrung des Tempelbergs
majeshi wa Israel katika eneo takatifu la msikiti wa Al-AqsaPicha: Getty Images/J. Guez

Kwa hakika vuguvugu la tatu la upinzani au 'Intifada' dhidi ya Israel linaonekana likiwadia.

Ni jambo ambalo Waisraeli wengi wanalihofia. Hofu hizi zinatokana na kuzidi kwa matukio tofauti ya vurugu kwa upande wa Wapalestina.

Katika kipindi cha wiki tatu zilizopita na kwa kupitia mashambulizi matatu tafauti, Wapalestina wamegonganisha magari yao na ya waisrael kwa makusudi na kuuwa mtoto mchanga, msichana mmoja kutoka Ecuador na polisi mmoja wa mpakani, pamoja na kujeruhi watu wengine 27.

Sio hayo tu, tukio lengine ni kupigwa risasi kwa myahudi mwenye msimamo mkali aliyekuwa akitetea haki za wayahudi wenziwe za kusali katika eneo takatifu la msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem, eneo ambalo tayari lina mgogoro.

Wapalestina pia wamezidisha vurugu kwa kumpiga visu hadi kufa askari mmoja wa Israel katika mji wa Tel Aviv, pamoja na mwanamke aliyekuwa katika maeneo ya ukanda wa Gaza.

Halikadhalika polisi wa Israel kwa upande wao, walimdunga risasi muandamanaji mmoja wa kipalestina katika mji wa Kiarabu ulioko kaskazini mwa Israeli. Tukio hilo lilitokea baada ya mwandamanaji huyo kushambulia gari la polisi hao.

Dunia sasa inaiangalia hali hii kwa macho ya wasiwasi – Je, vurugu hizi za mashambulizi mapya kweli zitaweza kudhibitiwa bila ya kuzuka vita?

Israel Siedlungsbau Har Homa Netanjahu 26.10.2014
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin NetanyahuPicha: Reuters/Abir Sultan

Tafauti na Ukanda wa Gaza - ambao kwa miaka kadhaa sasa unashuhudia mapigano yasiokwisha baina ya mashambulizi ya anga ya Palestina wakiwa wanajikinga na mashambulizi makali ya jeshi la Israel. West Bank, Jerusalemu, na miji kadhaa ya kiarabu ndani ya Israeli wao wamekuwa wakiishi kwa utulivu tangu baada ya vurugu za mapinduzi ya pili ya Intifada zilizomalizika mwaka 2005.

Waisraeli kwa mara nyengine tena wanajikuta wakiwa katika hali ya wasiwasi, na hofu ya uwezekano wa kuzuka vurugu kwa mara ya tatu.

Maafisa wametoa wito kuwa umma uwe macho.

Mazingira ya vurugu yatishia vuguvugu la upinzani la tatu

Wimbi la ghasia la hivi sasa linatokana na vurugu zilizoanza mwezi wa Juni na Julai mwaka huu. Kufuatia utekaji nyara na mauaji ya vijana watatu wa kiisrael na mmoja wa kipalestina. Vurugu ambazo zilisababisha vita vya siku 50 baina ya Israel na ukanda wa Gaza .

Mshauri wa zamani wa usalama, Yaakov Amidror, jana alijaribu kupunguza wasiwasi wa watu kwa kusema "Bado hatujafikia zile vurugu zilizoleta vuguvugu la mwanzo la upinzani ama Intifada ya mwaka 1987 au lile la pili.”

Lakini kwa upande mwengine mazingira yanaonekana kulingana na yale yaliyosababisha vuguvugu la upinzani wa pili la Septemba mwaka 2000. Wakati huo miongoni mwa sababu ziliyozusha hilo, ilikuwa ni ziara ya kiongozi wa zamani wa upinzani Ariel Sharon katika eneo takatifu la Jerusalem kitu ambacho hakijawapendeza wapalestina.

Na kwa mara nyengine tena eneo hilo takatifu kwa makundi yote mawili waisrael na wapalestina la msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem, limekuwa ndio chanzo cha kuleta vurugu.

Benjamin Netanyahu akanushashutuma za Wapalestina

Wapalestina wanawashutumu waisraeli kutaka kuvunja makubaliano yaliokuwapo kwa miongo kadhaa sasa, ya kuwa wayahudi wanaweza tu kutembelea eneo hilo lenye msikiti mtakatifu wa Al-Aqsa, lakini hawana ruhusa ya kusali katika msikiti huo ama eneo hilo.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alikanusha nia yoyote ya kubadili makubaliano hayo.

Aliongeza kwa kusema kuwa wito wa Wayahudi wenye msimamo mkali, wa kutaka haki za kuweza kusali katika msikiti huo wa Al-Aqsa au hata nia ya kuuvunja na badala yake kujenga hekalu la wayahudi hauwakilishi sera za serikali ya Israel.

Mwandishi: Yusra Buwayhid/DPAE

Mhariri: Mohammed Khelef