1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Palestina zaalikwa rasmi katika mkutano wa mashariki ya kati.

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQ2v

Washington. Marekani imezialika rasmi Israel na Palestina katika mkutano wa amani wa mashariki ya kati wiki ijayo. Kufuatia mazungumzo na rais Hosni Mubarak wa Misr , waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema kuwa mkutano huo wa amani mjini Annapolis utazungumzia masuala yote yanayohusika katika mzozo kati ya Israel na Palestina. Olmert amesema amani baina ya Israel na Palestina inawezekana kupatikana ifikapo mapema mwaka ujao.

Wakati huo huo waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ametoa ruhusa kwa mamlaka ya Palestina kupewa magari kadha ya deraya kama ishara ya mahusiano bora kabla ya mkutano muhimu wa amani unaodhaminiwa na Marekani. Magari hayo yaliyotengenezwa Russia yatakabidhiwa kwa mamlaka ya Palestina na Jordan na yatatumika katika eneo la kaskazini la ukingo wa magharibi katika mji wa Nablus, ambako mamia kadha ya polisi wa Palestina wamewekwa kwa idhini ya Israel kuanzia mwezi Novemba.