1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafungua mipaka yake na Gaza kwa mda

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvwG

GAZA:

Israel imefungua tena mipaka yake na Gaza, lakini kwa kiwango kidogo ili kukubali kupelekwa kwa mafuta,chakula na dawa katika ukanda wa Gaza.Hii ndio mara ya kwanza kwa Israel kulegeza mbinyo iliouwekea Gaza wiki jana kutokana na mashambulizi ya maroketi yakifanywa na waPalestina.Hata hivyo rais wa Israel Shimon Peres amesema kuwa jawabu katika mgogoro wa Gaza liko mikononi mwa Hamas.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa- umeonya kuwa mzingiro huo unaweza ukazusha janga la kibinadamu ,baada ya mtambo pekee wa kuzalisha umeme kulazimihswa kufungwa baada ya kuishiwa mafuta.kamishana wa masuala ya nje wa umoja wa Ulaya-Benita Ferrero Walder ameukosoa, mzingiro akisema kuwa ni adhabu kwa watu wote wa gaza hata na wale wasio na hatia.Na kwa mda huohuo,baraza la usalama la Umoja wa Mataifa- umeitisha kikao kujadilia hali inayozidi kuzorota katika eneo la Gaza. Hii imetokea baada ya kuombwa na wajumbe wa Kiarab katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.