1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yakubali kulegeza mbinyo wake kwa Gaza

28 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cyjb

JERUSALEM:

Waziri mkuu wa Isreal-Ehud Olmert- amekubali kulegeza vikwazo dhidi ya Gaza ili kuwezesha kupelekwa kwa mafuta katika eneo hilo,baada ya mkutano wake na rais wa Palestina- Mahmoud Abbas.Nchini Misri juhudi zinaimarishwa ili kufunga mpaka wa nchi hiyo na Gaza. Vikosi vya usalama vimeanza kuyazuia magari na pia kuimarisha ilinzi wake kuzunguka mji wa mpaka wa Rafah.Umoja wa Mataifa- unakisia kuwa kwa uchache wakazi laki saba wa Gaza ambao ni karibu nusu ya idadi yake yote, wamevuka mpaka wa Misri tangu wapiganaji wa Hamas kutoboa matundu katika ukuta utanaotenganisha Misri na Gaza siku ya jumatano ya wiki iliopita.Wengi wa wapalestina wanaoingia Misri, wanatafuta bidhaa mihumu,lakini Israel inahofia kuwa wapiganaji wa Hamas watatumia matundu hayo kuingiza silaha katika eneo la Gaza.