1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yapanga kufanya operesheni ya ardhini mjini Rafah

Amina Mjahid
10 Februari 2024

Mashambulizi ya angani ya Israel yameendelea katika mji wa Rafah wenye mkusanyiko mkubwa wa watu, baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutoa amri kwa wanajeshi kujiandaa kufanya operesheni ya ardhini huko

https://p.dw.com/p/4cFab
Israel | Benjamin Netanjahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Ohad Zwigenberg/AFP/Getty Images

Rafah ni eneo la kusini, ambalo limekuwa kimbilio la mwisho kwa wapalestina waliopoteza makazi yao. 

Benjamnin Netanyahu amepanga operesheni ya kijeshi ifanyike Rafah wanakoishi wapalestina wapatao milioni 1.3, baada ya kukimbia mapigano mjini Gaza.

Biden: Operesheni ya kijeshi ya Israel Gaza imepitiliza

Hatua hiyo imekosolewa vikali na makundi kadhaa ya kutetea haki za binaadamu pamoja na Marekani, wakati wapalestina wenyewe wakisema kwa sasa hawana mahali pengine pa kukimbilia. 

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema haiungi mkono operesheni hiyo mjini Rafah ikionya kwamba iwapo haitopangwa vizuri inaweza kusababisha janga kubwa.