1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yauwa Wapalestina wawili.

4 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CkEt

Gaza.

Majeshi ya Israel yamewauwa wapiganaji wengine wawili wa Kipalestina katika eneo la ukanda wa Gaza linalodhibitiwa na chama cha Hamas. Shambulio la hivi karibuni linakuja siku moja baada ya mashambulio kadha ya anga na ardhini kuuwa Wapalestina tisa katika eneo la Gaza. Operesheni hiyo ilianza baada ya wapiganaji wa Kipalestina kufyatua makombora upande wa mji wa kusini wa Ashkelon nchini Israel, ambao uko kilometa 17 kutoka ukanda wa Gaza. Rais wa Marekani George W. Bush anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza katika maeneo ya Israel na Palestina ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya mashariki ya kati baadaye mwezi huu.