1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yaendeleza mashambulizi kusini mwa Gaza

Grace Kabogo
19 Januari 2024

Israel imeendeleza mashambulizi kusini mwa Gaza baada ya kutofautiana hadharani na mshirika wake mkuu Marekani kuhusu uwezekano wa kuanzishwa taifa huru la Palestina.

https://p.dw.com/p/4bT3f
Wanajeshi wa Israel waendeleza mashambulizi ya ardhini huko Khan Younis
Wanajeshi wa Israel wakiendeleza mashambulizi ya ardhini katika mji wa Khan Younis, Ukanda wa GazaPicha: Ohad Zwigenberg/AP/picture alliance

Watu walioshuhudia mashambulizi hayo wamesema milio ya risasi na mashambulizi ya anga yalisikika mapema asubuhi huko Khan Younis, ambako Israel imesema wanamgambo wengi na viongozi wa kundi la Hamas wanajificha.

Shirika la Hilal Nyekundu la Palestina limeripoti kuhusu mashambulizi makali ya makombora karibu na hospitali ya Al-Amal.

Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza, imesema watu 77 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mapigano ya usiku kucha.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesisitiza kwamba vita dhidi ya Hamas vitachukua muda mrefu.