1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL: Gul ajiandaa kukutana na upinzani

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZE

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uturuki, Abdullah Gul, ameahidi kuheshimu katiba ya nchi iwapo atachaguliwa na bunge kuwa rais.

Gul anajiandaa kukutana na viongozi wa upinzani kupata uungwaji mkono katika juhudi zake za kutaka kuwa rais wa Uturuki.

Waziri Gul amewasilisha rasmi ombi lake kwa bunge kuwania wadhifa wa urais baada ya chama chake cha AK kumteua agombee kwa mara ya pili.

Uteuzi wake mnamo mwezi Aprili mwaka huu ulisababisha maandamno katika miji mikubwa nchini Uturuki na kumlazimu waziri mkuu, Recep Tayyip Erdowan, kuitisha uchaguzi wa mapema.

Waturuki wasio na msimamo mkali wa kidini, wakiwemo pia majenerali wa jeshi la Uturuki, wanahofia chama cha AK kinapania kuvuruga utulivu uliopo baina ya taifa na dini katika nchi hiyo iliyo na idadi kubwa ya waislamu. Chama cha AK kimeendelea kupinga madai hayo.