1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL: Merkel akamilisha ziara yake ya Uturuki leo

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5d

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel anakamilisha ziara yake rasmi nchini Uturuki hii leo. Bi Merkel anatarajiwa kukutana na viongozi wa kidini na kibiashara mjini Instanbul.

Hapo jana alifanya mazungumzo na waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan mjini Ankara, kabla kusafiri pamoja naye kwenda Instabul. Akizungumzia kuhusu uhusiano kati ya Ujerumani na Uturuki Bi Merkel alisema,

´Ninafikiri tunaweza kusema uhusiano kati ya Ujerumani na Uturuki umekaribiana sana na ni wa kirafiki. Tulikutana mara ya mwisho nchini Ujerumani tarehe 26 mwezi Mei na sasa kama kansela wa Ujerumani niko hapa kwa mara ya kwanza. Na ninayo furaha kwamba tutaweza kuendelea kuyajadili kwa kina maswala mbalimbali.´

Kansela Merkel ameishauri Uturuki ikamilishe masharti ya Umoja wa Ulaya na ifungue bandari zake kwa sehemu ya Cuprus inayomilikiwa na Ugiriki, ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Lakini waziri mkuu Erdogan amesema Umoja wa Ulaya lazima kwanza uondoe kiwakzo cha kibiashara dhidi ya sehemu ya Cyprus inayomilikiwa na Uturuki.