1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL: Mwandsihi wa habari azikwa leo

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYb

Maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa kidini wa Armenia na wanadiplomasia wa kigeni wanatarajiwa hii leo kuhudhuria mazishi ya mwandishi wa habari aliyekuwa raia wa Uturuki mwenye asili ya kiarmenia, Hrant Dink, aliyeuwawa kwa kupigwa risasi. Maofisa zaidi wa polisi wametumwa kushika doria katika eneo anakozikwa.

Dink atazikwa katika makaburi ya Waarmenia baada ya ibada nje ya ofisi ya gazeti alilolianzisha. Wakati huo huo, polisi wa Uturuki wamepanua uchunguzi wao juu ya uhusinao baina ya mvulana wa miaka 17 aliyekiri alimuua mwandishi wa habari Hrant Dink na kundi lenye siasa kali za kizalendo nchini Uturuki.

Dink aliyaeleza mauaji ya Waarmenia yaliyofanywa wakati wa enzi ya ufalme nchini Uturuki mwanzoni mwa karne hii kuwa mauaji ya halaiki, hatua ambayo iliwafanya wazalendo wenye siasa kali kumuita haini.