1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL : Saba wahukumuiwa kifo kwa kuripua mabomu

17 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRR

Mahkama ya Uturuki imewahukumu watuhumiwa saba wanamgambo wa kundi la Al Qaeda kifungo cha maisha gerezani kwa dhima yao katika uripuaji wa mabomu mjini Istanbul hapo mwaka 2003 uliouwa takriban watu 60.

Mashambulizi hayo yalilenga mahekalu mawili ya Kiyahudi ubalozi mdogo wa Uingereza na tawi la benki moja yenye makao yake makuu mjini London.Watuhumiwa wote wanashutumiwa kwa kuunda kitengo cha watu wa itikadi kali nchini Uturuki chenye mafungamano na kundi la Al Qaeda.

Watu hao saba ni miongoni mwa zaidi ya watuhumiwa 70 kufikishwa mahkamani kuhusiana na mashambulizi hayo.