1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Istanbul. Waasi wa PKK kukamatwa nchini Iraq.

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7A4

Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki ameahidi kuwakamata viongozi wa waasi wa Kikurdi wanaohusika na mashambulizi katika mpaka wa Uturuki wakitokea kaskazini mwa Iraq.

Katika mkutano wa kimataifa wa usalama mjini Istanbul , al-Maliki ameahidi kufunga ofisi za vyama vilivyo na uhusiano na chama cha wafanyakazi wa Kikurdi , cha PKK. Pia ametoa wito kwa mataifa jirani ya nchi hiyo kuimarisha ulinzi katika mipaka yao.

Marekani pia imeahidi kuisaidia Uturuki katika mapambano yake dhidi ya PKK.