1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Istanbul. Wanajeshi wa Uturuki waachwa huru na PKK.

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79z

Wapiganaji wa Kikurdi wanaripotiwa kuwa wamewaacha huru wanajeshi wanane wa Uturuki ambao waliwakamata wiki mbili zilizopita katika shambulio la kushtukiza karibu na mpaka na Iraq. Msemaji wa chama cha PKK, amesema kuwa wanajeshi hao wamekabidhiwa kwa maafisa wa Kikurdi nchini Iraq. Hii inakuja siku moja baada ya serikali ya Iraq kuchukua hatua dhidi ya waasi wa PKK ambao wanashambulia ardhi ya Uturuki kutoka katika maficho yao kaskazini mwa Iraq.

PKK wameongeza kampeni yao ya kijeshi mwezi uliopita , na kuleta kitisho cha Uturuki kulipiza kisasi kijeshi.